Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhani amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar baada ya kuugua maradhi ya moyo.

Familia yake imesema hali ya Jaji Ramadhani ilibadilika jana usiku na kukimbizwa hospitalini hapo ambapo mauti ilimkuta leo asubuhi.
 
Jaji Augustino Ramadhani pia alikuwa Brigedia Jenerali kabla ya kuitwa katika sekta ya Sheria na kutumikia Mahakama.

Alipostaafu ujaji, alipewa kazi ya ukasisi, akatawazwa rasmi kuwa Mchungaji wa Dayosisi ya Kanisa la Anglikana lililopo Mkunazini Zanzibar na hivyo kuitwa “Mchungaji Augustino Ramadhani”