Aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Mafia (2005-2015), Abdulkarim Shah (59) amefariki dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Hindu Mandal, jijini Dar as Salaam.

Akiwa mbunge, Shah alipata kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na pia alikuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi ya Bunge.

Marehemu Abdulkarim Shah atazikwa leo Aprili 26, 2020 sasubuhi katika makaburi ya Kisutu jijini Dar