Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza kupona kwa wagonjwa wawili zaidi wa virusi vya Corona na hivyo kufanya idadi ya waliopona ugonjwa huo kufikia watano.

Wagonjwa waliopona ni kutoka Dar es Salaam na Arusha. “Takwimu za leo kutoka maabara kwa waliochukuliwa sampuli hakuna maambukizi, wenye corona Tanzania wanabakia 24, Zanzibar 7 na Bara 17, leo tumepata wagonjwa wawili ambao wamepona, wa DSM na Arusha(jumla TZ wamepona watano), kwahiyo sasa hatuna mgonjwa corona Arusha na Kagera”-Waziri wa Afya Ummy Mwalimu

The post Tanzania: Waliopona Virusi vya Corona wafikia Watano appeared first on Bongo5.com.