New Zealand inasema kwamba imezuia maambukizi ya Covid 19 katika jamii hatua ambayo inamaanisha kwamba wameangamiza virusi hivyo.

Huku wagonjwa wapya wachache wakiripotiwa katika siku kadhaa – mmoja siku ya Jumapili – Waziri mkuu Jacinda Ardem amesema kwamba virusi hivyo vimeangamizwa kabisa.

Lakini maafisa wameonya dhidi ya kupunguza kasi dhidi ya virusi hivyo, wakisema kwamba haimaanishi kwamba visa vya ugonjwa huo vimeisha kabisa.

 

Habari hiyo inajiri saa chache kabla ya New Zealand kuondoa masharti yake makali ya kukaribiana miongoni mwa raia wake.

Kuanzia Jumanne , biashara zisizo na muhimu mkubwa , huduma za Afya na elimu zinatarajiwa kufungua milango yake tena.

Watu wengi hatahivyo watatakiwa kusalia majumbani kila wakati na kuzuia kukaribiana.

“Tunaufungua uchumi , lakini haturuhusu mikusanyiko ya watu” , bi Arden alisema katika hotuba hiyo ya serikali ya kila siku kwa umma. News Zealand imeripoti chini ya wagonjwa 1,500 na vifo 19 .

Mkurugenzi mkuu wa Afya nchini New Zealand Ashley Bloomfield alisema kwamba wagonjwa wachache wanaoripotiwa katika siku za hivi karibuni wanatupatia motisha kwamba tunaafikia lengo letu la kuangamiza ugonjwa huu.

Waziri mkuu wa NZ Jacinda ArdernHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWaziri mkuu Jazinda Ardern alisema kwamba New Zealand haiwezi kusema jinsi hali ingeweza kuwa bila amri ya kutotoka nje.

Je New Zealand ilikabiliana vipi na virusi hivyo?

Taifa hilo liliweka baadhi ya masharti makali zaidi duniani kuhusu usafiri na kukabiliana na virusi hivyo wakati ilipothibitisha wagonjwa wachache.

Ilifunga mipaka yake, na kuanza kuweka masharti ya karantini , kutoa amri ya kutotoka nje mbali na kuanzisha vipimo vya umma na kuwasaka walioambukizwa.

Fukwe za bahari na maeneo ya michezo yalifungwa tarehe 26 mwezi Machi pamoja na ofisi na shule.

Klabu za burudani na mikahawa pia ilifungwa ikiwemo kununua chakula na kuletewa nyumbani.

Bi Ardern anasema kwamba New Zealand ingeweza kuripoti wagonjwa 1000 kwa siku iwapo hakuchukua hatua hizo za haraka na mapema .

Anasema taifa hilo halijui jinsi hali hiyo ingeweza kuwa mbaya , lakini kupitia majadiliano wamefanikiwa kuzuia maafa mabaya zaidi.

Lakini pia serikali imepongezwa kwa jumbe zake za wazi wakati wa mlipuko huo wa virusi.

NZ iliweka masharti makali ikiwemo kufunga klabu za burudani mapema wakagti wa mlipuko huo.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNZ iliweka masharti makali ikiwemo kufunga klabu za burudani mapema wakagti wa mlipuko huo.

Ifikiapo mwendo wa saa sita usiku siku ya Jumatatu taifa hilo litapunguza masharti ya amri ya kutotoka nje kutoka awamu ya nne hadi ya tatu.

Hiyo inamaanisha kwamba biashara zitafunguliwa – ikiwemo mikahawa lakini sio zile zinazohusisha watu kuonana ana kwa ana.

Mikusanyiko ya umma bado imepigwa marufuku na watoto wengi hawatakwenda shule . Mpaka wa New Zealand utasalia umefungwa.

Je ni nini kinachoendelea Australia?

Nchini Australia ongezeko la maambukizi limepungua kwa kiasi kikubwa katika wiki za hivi karibuni. Kulikuwa na wagonjwa wapya 16 walioripotiwa siku ya Jumapili.

Sawa na New Zealand , serikali yake imepongezwa kwa hatua zake kukabiliana na tatizo hilo na kura ya maoni inaonesha kwamba uaminifu kwa uongozi umeongezeka.

Masharti makali yameanza kupunguzwa katika baadhi ya maeneo , huku baadhi yao yakipanga kuondoa masharti ya kutokaribiana ili kuruhusu watu kujitokeza katika maeneo ya umma wiki hii.

Katika eneo la Queensland kuanzia siku ya Jumamosi , watu wataruhusiwa kwenda madukani ,kujivinjari katika bustani kuogelea baharini iwapo eneo hilo halipo umbali wa dakika 40 kutoka nyumbani.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

The post Taifa la New Zealand limetangaza namna lilivyoangamiza virusi vya Corona “Hatuna mgonjwa mpya” appeared first on Bongo5.com.