Vyombo vya habari nchini Syria vimeripoti kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya nchi hiyo imeyadungua makombora kadhaa ya Israel katika mji wa kihisotria wa Palmyra uliopo kwenye jimbo la Homs.

Shirika la Habari la Syria SANA limearifu kuwa Syria imefanikiwa kudhibiti uchokozi wa Israel baada ya kuyaangusha makombora yake kabla ya kufika kwenye maeneo yaliyolengwa.
Shirika linalofuatilia Haki za Binadamu nchini Syria limesema, makombora hayo yalivilenga vituo vya kijeshi vinavyotumiwa na wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran kwenye jangwa la Palmyra.
Tangu kuanza kwa mzozo wa Syria mwaka 2011, Israel imefanya mamia ya mashambulizi ya anga nchini Syria ikivilenga vikosi vya serikali pamoja na vile vya washirika wake wa Iran na wapiganaji wa kundi la Hezbollah.
The post Syria yasema imedungua makombora ya Israel appeared first on Bongo5.com.