Ilianza S5 na S5 lite, sasa Infinix Mobile inakuletea S5 pro, ikiwa na sifa lukuki zinazo ipa umaridadi zaidi.


S5 pro imekuja na Android version 10 na utofauti mkubwa katika upande wa kamera na kuifanya kuwa simu ya kwanza yenye muonekana wa kuvutia na kamera kali zaidi kwa kulinganisha na simu za awali katika toleo la “S Series”.

Selfie kamera ya S5 Pro inasemekana ina megapixel si chini ya 40 zenye kujichomoza kwa juu wakati wa upigaji selfie, na inasemekana haichuji wala kupoteza ubora yaani unaweza kupiga Picha (kujiselfisha) hata mara 500 kwa siku na ubora uko pale pale.

Hii ni zaidi ya maajabu kwenye Simu hii Kutoka Infinix Mobile na wadau wa Infinix kupitia mtandao wa kijamii wa infinixmobiletz wameonekana kuisubiri kwa hamu.

The post Simu nyingine yenye kamera ya maajabu kutoka Infinix kuingia sokoni muda si mrefu appeared first on Bongo5.com.