Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema kuwa ipo haja Simba SC kupewa Kombe la Ligi Kuu soka Tanzania Bara kama hali itaendelea kuwa hivi, kwa dunia kuendelea kupambana na janga la Virusi vya Corona.

Kupitia kipindi cha Sports Arena cha Wasafi Tv, Rage ambaye amejizoelea umaarufu Mkubwa zama za utawala wake ametolea mfano ligi ya Ubelgiji ‘Jupiter Pro League’ ambapo wiki chache zilizopita Club Brugge ilikabidhiwa Ubingwa kwa msimu wa mwaka 2019/20 mara baada ya Bodi ya Wakurugenzi kukubaliana.

Kama hali inaendelea kuwa hivi, kuhusu Corona kwenye taratibu za FIFA, hali kama hii, hili gonjwa lilipotokea hakuna mwanadamu aliyetegemea na ni janga la Kimataifa, ni vyema tukafanya kama walivofanya Ubelgiji.”

”Ligi imesimamishwa, aliyekuwa anaongoza anaongoza, aliyekuwa anashuka daraja anashuka, kama hali itaruhusu tunaweza tukaendelea na ligi. Utaratibu mzuri ni TFF wawasiliane na CAF ili wajue na wao ligi yao ya Klabu bingwa na kombe la Shirikisho linaanza lini.”

”Mimi nashauri bwana Simba iwakilishe klabu bingwa, Azam FC ituwakilishe FA Cup na Yanga iwakilishe Mbuzi Cup,” Amemalizia Aden Rage huku akicheka na kudai kuwa kwake Yanga ni watani wake.

The post ”Simba apewe Ubingwa, Azam ashiriki FA Cup, Yanga atuwakilishe Mbuzi Cup”- Aden Rage (+Audio) appeared first on Bongo5.com.