Shirika la Afya Duniani – WHO limesema hapo jana kuwa ushahidi wote uliopo unadokeza kuwa virusi vya corona vilitoka kwenye wanyama nchini China mwishoni mwa mwaka jana na havikutengenezwa katika maabara.

Msemaji wa WHO Fadela Chaib ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Geneva kuwa kuna uwezekano mkubwa vilitoka kwenye popo lakini bado haijagundulika virusi hivyo vilitoka vipi kwenye popo na kuingia kwa binaadamu.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema wiki iliyopita kuwa serikali yake inajaribu kubaini kama virusi hivyo vilitengenezwa kwenye maabara katika mji wa Wuhan nchini China, ambako janga la virusi vya corona lilianzia Desemba mwaka uliopita.

The post Shirika la Afya Duniani (WHO) lataja Virusi vya Corona vilipotoka appeared first on Bongo5.com.