Shirika la Afya Duniani WHO limeonya kuwa mzozo wa virusi vya corona hautamalizika hivi karibuni kutokana na mataifa mengi kuwa kwenye hatua za mwanzo za kupambana na virusi hivyo hatari.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus amesema itakuwa ni kosa kubwa kuharakisha kuondowa haraka vizuizi vya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona kwa sababu hali bado haijatengamaa.

Ghebreyesus ameongeza kusema wakati mataifa mengi yako katika siku za mwanzo za mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, nchi zilizoathiriwa mapema zinashuhudia wimbi jipya la maambukizi.

Mkuu huyo wa shirika la WHO pia ameendelea kuhimiza umuhimu wa kuwepo mshikamano duniani katika vita dhidi ya virusi vya corona

“Na iwapo kutakuwa na mshikamano wa ulimwengu, na kuichukulia kadhia hii kuwa adui wa wote wa ubinadamu na kujitoa kikamilifu huku tukitambua kwamba kirusi hiki ni kipya na ni hatari – tunaweza kushinda.

Bila ya hilo, bila ya umoja wa kitaifa na mshikamano wa kimataifa, tunawaambiene hali mbaya zaidi iko mbele yetu.

Kwa pamoja tuzuie janga hili.” amesema Ghebreyesus

The post Shirika la Afya Duniani laonya kuhusu virusi vya corona  appeared first on Bongo5.com.