Serikali ya Rwanda imeogeza kwa karibu wiki mbili amri ya kutotoka nje hadi Aprili 30 kama sehemu ya hatua ya kudhibiti kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Hii ni hatua ya pili kali kutangazwa na serikali wiki mbili baada ya amri ya kwanza ya kutotoka nje kutangazwa ghafla usiku wa Machi 21 na kuanza kutekelezwa asubuhi yake.

Wakati huo Rwanda ilikuwa imeripoti kuwa na wagonjwa 17 pekee wa orona, lakini idadi hiyo siku ya Ijumaa iliongezeka hadi 138, huku watu 60 wakithibitishwa wakipona.

Hakuna mtu aliyeripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19 nchini Rwanda.

Watu wanaruhusiwa kutoka majumbani mwao wakati wanapoenda kutafuta huduma za kimatibabu,chakula, huduma za kifedha au kutoa huduma hizo.

Wafanyabiashara wadogo wameathiriwa zaidi na hatua hiyo; baadhi yao wamesimulia BBC jinsi maisha yalivyokuwa magumu wiki mbili za kwanza.

Mamlaka nchini Rwanda imesema kuwa itaendelea kutoa msaada wa chakula kwa watu wasiojiweza japo idadi ya watu hao imekuwa kubwa zaidi.

The post Rwanda waongeza siku 14 za kuendelea kukaa ndani kujikinga na corona appeared first on Bongo5.com.