Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Anna Mghwira ametangaza kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo siku tatu zilizopita.

Mama Anna Mghwira, amesema kuwa hakuwahi kujisikia dalili zozote zile za Corona, bali aliamua kwenda kupima tu ili ajue afya yake na kujikuta ameambukizwa.

Mama Mghwira amesema anaendelea vizuri, huku akisisitiza watu waendelee Kujikinga na Maambukizi kwa kufata maelekezo ya wizara ya Afya na Wataalamu.

Chanzo Cloudstv

The post RC Kilimanjaro ajitangaza kuwa na virusi vya Corona “Niliamua kupima sikuwa na dalili zozote” appeared first on Bongo5.com.