Kwa mujibu wa jarida la @forbes, Kanye West ana utajiri wa Dola Bilioni $1.3 na kumfanya kuwa msanii wa Hip Hop mwenye mkwanja mrefu zaidi kwa mwaka 2020.

Asilimia kubwa ya mkwanja huo, Kanye West amesema unatokana na biashara yake ya viatu Yeezy sneakers.

Awali Kanye West aliwapa Forbes document zake zote za mauzo ya viatu, Na majumuisho yalikuwa ni Dola Bilioni $3.2 kabla ya makato yote kufanyika.

Kanye West anakuwa msanii wa pili wa Hip Hop kuwa Bilionea, Baada ya Jay-Z kutawala kwa muda mrefu.

Hata hivyo, Kanye West bado anadai kuwa yeye ni Bilionea tangu muda mrefu ila hakutaka kuwaanisha Forbes kwa kuwapa nyaraka za mauzo ya viatu vyake.

Kama utakumbuka, mwaka jana jarida la Forbes lilimtaja Kanye West kuwa ana utajiri wa ($890m), kitu ambacho kilimkasirisha Kanye na hakukiunga mkono kabisa kwani alisema yeye ni bilionea na ana utajiri wa ($3 billion)

Kwa mujibu wa taarifa mpya iliyotoka jana Ijumaa, Forbes wamempa Kanye hadhi ya Bilionea wakidai ana utajiri wa ($1.3 billion) ambazo ni zaidi ya Trilioni 3 za Kitanzania.

The post Rasmi Kanye West atajwa kuwa bilionea na kuwa Rapper wa pili baada ya Jay Z appeared first on Bongo5.com.