Rais Jair Bolsonaro wa Brazil ameamua kujiunga na mamia ya waandamanaji nje ya makao makuu ya jeshi mjini Brasilia kupinga amri ya kubakia nyumbani iliyotangazwa na magavana wa majimbo nchini humo.
Kundi la waandamanaji zaidi ya 600 lilipiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi la nchi hiyo jana Jumapili April 19, 2020 likipinga amri ya kusalia majumbani ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Corona.

Rais Bolsonaro aliwaambia waandamanaji kuwa amejiunga pamoja nao kwa sababu anakubaliana na mawazo wanayotoa.
Hata hivyo taifa hilo la Brazil lina idadi kubwa ya maambukizi ya Virusi vya Corona katika eneo la Amerika ya Kusini. Waliombukizwa hadi sasa ni 38,000 huku vifo vikiwa ni 2400.
Hata hivyo taifa hilo la Brazil lina idadi kubwa ya maambukizi ya Virusi vya Corona katika eneo la Amerika ya Kusini. Waliombukizwa hadi sasa ni 38,000 huku vifo vikiwa ni 2400.
Mara kadhaa kiongozi huyo amekosoa hatua zilizochukuliwa na magavana za kuweka vizuizi vya wastani ikiwemo kwenye miji yenye idadi kubwa ya watu ya Sao Paulo na Rio de Janeiro ili kuzuia kusambaa virusi vya corona.