Hapo jana Rais Jair Bolsonaro wa Brazil alijiunga na mamia ya waandamanaji nje ya makao makuu ya jeshi mjini Brasilia kupinga amri ya kubakia nyumbani iliyotangazwa na magavana wa majimbo nchini humo.

Brazil's Bolsonaro joins protest against stay-at-home orders

Rais Bolsonaro aliwaambia waandamanaji kuwa amejiunga pamoja nao kwa sababu anakubaliana na mawazo wanayotoa. Hata hivyo taifa hilo la Brazil linaidadi kubwa ya maambukizi katika eneo la Amerika ya Kusini.

Mara kadhaa kiongozi huyo amekosoa hatua zilizochukuliwa na magavana za kuweka vizuizi vya wastani ikiwemo kwenye miji yenye idadi kubwa ya watu ya Sao Paulo na Rio de Janeiro ili kuzuia kusambaa virusi vya corona.

The post Rais wa Brazil Jair Bolsonaro ajiunga na waandamanaji kupinga amri ya kubaki nyumbani kisa Corona appeared first on Bongo5.com.