Rais wa Marekani Donald Trump amesema nchi yake imefikia kilele cha kupata visa vipya vya ugonjwa wa COVID-19 na kutabiri kuwa baadhi ya majimbo yataondoa marufuku ya kutotoka nje na kurejea katika hali ya kawaida mwezi huu.

Katika maelezo yake ya kila siku White House kuhusu ugonjwa huo, Rais Trump amesema muongozo mpya wa kurejelea shughuli za kawaida utatangazwa leo Alhamisi baada ya kuzungumza na magavana.

Rais Trump alinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo akisema “Tutarejelea hali ya kawaida wanangu, tena sisi sote, twataka nchi yetu tena.”

Marekani ina takribani watu 638,000 waliothibitishwa kuwa ugonjwa wa COVID-19 na zaidi ya vifo 30,800.

Rais Trump hapo jana Aprili 15, 2020 aliwaambia waandishi wa habari kuwa takwimu za kitaifa zinaashiria nchi yake imepita kilele cha maambukizi mapya ya virusi vya corona, hivyo anatumaini taifa lake litaendelea hivyo, kupiga hatua zaidi ya kuepusha maambukizi mapya mengi.

The post Rais Trump adai Marekani imefika kilele cha maambukizi mapya ya corona appeared first on Bongo5.com.