Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Wabunge na Waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto kufuatia kifo cha Mhe. Askofu Getrude Rwakatare.

“Katika kipindi hiki cha majonzi tumuombee askofu Rwakatare apumzike mahali pema peponi na nawasihi waumini wa kanisa la Mlima wa moto muendelee kuwa wamoja na muendeleze mazuri yote yaliyofanywa na Askofu Rwakatare wakati wa uhai wake”

Mbali na ujumbe huo wa Rais Magufuli pia Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassani pia ametuma salamu hizi:-

“Kwa Masikitiko na Mshtuko nimepokea taarifa ya kifo cha aliyekuwa Askofu na Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God) na Mbunge wa Viti Maalum CCM Mhe. Dr. Gertrude P Lwakatare kilichotokea leo April, 20,2020, namuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu peponi na amjaalie Upepo wa Kisulisuli Amin.”

 

The post Rais Magufuli, Mama Samia Suluhu watuma salamu za rambirambi kwa familia ya Rwakatare appeared first on Bongo5.com.