Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Familia,Wabunge na Waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto kufuatia kifo cha Askofu Getrude Rwakatare.

Rais Magufuli amesema Askofu Rwakatare alikuwa Mcha Mungu, mwenye upendo, asiye na majivuno, aliyepigania umoja na amani na aliyeipenda Tanzania.