Michael Lane Brandin aliambiwa kwamba ujumbe wake aliotuma kwenye mtandao wa Facebook utasababisha hisia tofauti.

Kile ambacho hakufahamu ni kwamba atakamatwa, atapoteza kazi na kushtakiwa kwa makosa ambayo huenda yakamfanya akajipata kizimbani.

Ilikuwa ni majira ya mchana mwezi Machi na mjadala kuhusu namna ya kukabiliana na Covid-19 ulipokuwa unaendelea kila mahali.

Hivyo yeye, akaamua kushiriki mjadala huo kwa kuandika.

Michael alituma ujumbe unaosema kwamba yeye amepatikana na virusi vya corona na madaktari walikuwa wamemuambia kuwa virusi hivyo vinaweza kusambazwa kwa njia ya hewa.

Kupitia mtandao wa Facebook, alichokutana nacho hakuamini, kuhurumiwa na mshtuko. Rafiki zangu walimtumia ujumbe kumuuliza kama yuko sawa, na akasema yuko sawa, katika ujumbe wake alikuwa anatania tu,’ anasema.

Kipi kilikuwa kinaendelea kando na mtandao hangewahi kukifikiria.

Uvumi tayari ulikuwa umeanza kusambaa kama moto wa msituni katika kaunti yote ya Tyler. Kulingana na polisi katika mji wa Texas, tayari watu walikuwa wameanza kuwa na wasiwasi.

Huo ni wakati ambapo hakuna nchi yoyote ambayo ilikuwa imetoa amri ya kutotoka nje kwa raia wake na pia walikuwa wanapiga simu hospitali uuliza ikiwa taarifa hizo zilikuwa za kweli na kile ambacho wanaweza kufanya kujilinda.

Kibali cha kukamatwa

Polisi ikawasiliana na Michael na kumwambia kwamba arejee kwenye ujumbe wake wa Facebook na kuandika tena kwamba alichokisema hakikikuwa cha kweli na akafanya hivyo.

Hatahivyo, uvumi huo ulikuwa unaendelea kusambaa na ujumbe mwingine katika ukurasa wa Facebook ukawa unatoka kwenye akaunti ya Tyler ofisi ya Sheriff:

‘Katika lalamiko rasmi kutoka idara ya makosa ya jinai, hakimu Jacques Blanchett alitoa kibali cha kukamatwa kwa Brandin kwa makosa ya kuzua taharuki kwa taarifa za uwongo.

Brandin akajipeleka kwa mamlaka.

‘Nilijipeleka mwenyewe na baada ya mchakato wa kujiandikisha kukamilika, wakasema kwamba usiko huo nitalala jela kwasababu ni lazima nimsubiri hakimu siku itakayofuata.

Nilikuwa na wasiwasi kupita maelezo,’ Brandin anasema.

Kwasasa amerejea nyumbani akisubiri siku ya kesi yake kusikizwa ambayo hadi kufikia sasa haijulikani kwasababu ya kusambaa kwa virusi vya coona lakini licha ya kwamba hali ilivyo kwa Brandin bado ni tete, anasema kwamba bado anahisia mchanganyiko kuhusu ikiwa anajutia kile alichofanya au la.

Michael Lane Brandin school photo

‘Nina shahada ya uanahabari na nimesomea nyanja hiyo kuonesha vile ilivyo rahisi kwa yeote yule kutuma ujumbe mtandaoni na kusababisha wasiwasi. Pia nilitaka kudhihirisha kwamba ni muhimu kwa watu kuelimika na kufanya utafiti wao kabla ya kukubali kwamba kila wanachokisoma mtandaoni ni cha kweli.

Lakini kwa ujumbe nilioandika Facebook, nimepoteza kazi, mafao yangu ya afya, na pia sikuweza kuanza shahada yangu ya uzamili kwa wakati niliokuwa nimepanga kwa ukosefu wa pesa na hilo limeniongezea mzigo wa kifedha kwa familia yangu kwasababu wote wananisaidia kulipa gharama zangu.

‘Licha ya kwamba najutia, nililazimika kuandika barua ya kuacha kazi na kulala jela kwa usku mmoja na pia ama naweza kuambiwa nilipe faini au hata kuhukumiwa kifungo jela. Hayo sio mambo mazuri.’

Katika ofisi ya umma, wamesema wamelazimika kuchukua hatua hiyo kwasababu ya wasiwasi uliokuwa unaendelea kuhusu virusi vya corona Marekani

Marekani sio eneo pekee ambapo ambapo sheria mpya inamaanisha kusambaza taarifa kwa mitandao ya kijamii kuhusu virusi hivyo kunaweza kukufanya ukakamatwa.

Watu waliokamatwa kote duniani

Waliokamatwa kwa kusambaza taarifa za uongo ni taarifa zinazoripotiwa India, Morocco, Thailand, Kenya, Cambodia, Somalia, Ethiopia, Singapore, Botswana, Russia na Afrika Kusini.

Katika baadhi ya matukio, uvumi unaweza kusambaa ukiwa na nia njema lakini waangalizi wa haki za Binadamu wametuambia wamesema kwamba wana wasiwasi kuwa janga hili limefanya mafia kuwa na nguvu mno kiasi cha kukandamiza wale wanaowakosoa.

Nchini Kenya, Robert Alai pia nawe ameachiliwa kwa dhamana na anakabiliwa na mashtaka ambayo huenda yakamfanya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwasababu ya virusi vya corona kupitia mtandao wa Twitter.

Picture of the jail cell

Tayari aliwahi kuwa kizuizini kwa siku 3 kwa ujumbe uliodai kuwa amesikia kwamba kuna mlipuko wa ugonjwa huo katika bandari ya Mombasa.

Kulingana na mamlaka, hatua hiyo ilichukuliwa kwa kuzingatia kifungu cha sheria cha matumizi mabaya ya kompyuta na uhalifu wa kimtandao 2018.

Bwana Alai alikamatwa siku kama ya Ijumaa nakusalia kizuizini wikendi hadi pale hakimu alipoonekana. Bwana Alai anadai kwamba hatua ya kutokaribiana haikutimizwa wakati akiwa amekamatwa hadi alipozungumzia suala hilo.

‘Nililala kwenye sakafu pamoja na wengine wengi tu. Sikupewa barakoa ya kujinga ama kitu kingine kile cha kujikinga.

Tulipima chumba ambacho tulikuwa tumezuiliwa kwa kutumia programu ya kupima kwenye simu aina ya iPhone na kubaini kwamba ukubwa wake ulikuwa wa mita 4 kwa mita 3 na kulikuwa na watu wengi ambao sikuweza kuwakalisha chini.

Huwezi kunikamata kwasababu y kuhatarisha maisha a uniweke namna ile wakati wa janga kama hili. Tulilalamika na hatimae tukagawanywa.’

Picture of Robert Alai

Bwana Alai anafahamika kwa kuwa mwanablogu mwenye kupinga serikali akiwa na wafuasi karibia milioni 1 kwenye mtandao wa Twitter.

Polisi bado hawajajibu ombi la kutaka kuzungumza na BBC lakini walituma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter siku 5 kabla ya kukamatwa kwake kuhusiana na kesi inayofanana na hiyo.

Mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa kesi za uhalifu Kenya, alisema kuwa kuna mwanamme mmoja ambaye amekamatwa eneo la Mwingi kwa kuchapisha taarifa zenye kupotosha kuhusu virusi vya corona… atashtakiwa kwa kuchapisha taarifa za uwongo ambazo zinasambaa na kusababisha wasiwasi tofauti na kifungi cha 23 cha sheria ya utumizi mbata wa Kompyuta.

Mamlaka nchini Kenya imerejelelea ujumbe wake kwa jamii wa kutosambaza taarifa za uwongo na uvumi. Siku kabla ya Bwana Alai kukamatwa, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema: “Uvumi huu ni lazima ukome… lakini kwasababu najua kusema kwa mdomo tu hakutoshi, tutakamata kadhaa ili kudhihirisha kile tunachosema.”

Bwana Alai anaamini kwamba taarifa alizopewa zilikuwa za kweli na kwamba hakuna sheria aliyovunja, ingawa BBC imeshindishwa kuthibitisha madaia yake.

Bwana Alai amekamatwa kwa kutoa matamshi ya kutatanisha mara nyingi tu kabla ya tukio la hivi karibuni, lakini amefikiria kwamba polisi wanatumia janga hilo kuandama wakosoaji wake.

‘Wamekamata wanablgu wengine kwa makossa kama hayo na kwangu mimi naona kuwa ujumbe wowote wa Twitter kuhusu virusi vya corona au katika mtandao mwingine wowote ule wa kijamii, kwasasa kunachukuliwa kama kosa la uhalifu. Sisemi kwamba wasikamate watu lakini naona ni muhimu polisi kufanya kazi yao ila wanastahili kuandama wale wakosaji. Watu wana haki ya kufahamishwa na mimi ni haki ya kujieleza,’ alisema.

Iwapo atapatikana na hatia, Bwana Alai anakabiliwa na faini ya milioni 5 za Kenya au kifungo cha miaka 10 jela. Anasema kwamba mke wake na watoto wana wasiwasi kuhusu hatma yao lakini anasema kuwa amedhamiria kuendelea kuzungumzia virusi vya corona mtandaoni.

Wengi wamekamatwa India

Hali kama hiyo inaendelea nchini India ambapo Sikandar Cuttrack anasubiri hukumu yake kwa kuhoj mamlaka ya eneo kwenye Twitter.

Nimejaribu tu kufahamisha polisi na utawala kuhusu mgojwa aliyekuwa anashukiwa kuwa na covid-19,’ anasema.

Sikandar Cuttrack in the streetSikandar Cuttrack alituma katika mtandao wa Twitter kuhusu virusi vya corona mjini anakotokea

‘Nimetuma ujumbe mara kadhaa na polisi wakanikamata wakisema kwamba nimesababisha hali ya wasiwasi miongoni mwa umma.

Sikuhisi kwamba nimefanya makosa yoyote. Naamini kwamba polisi wamechukua hatua stahili. Hali ya corona imefanya polisi kuwa na nguvu zaidi. Wanafanya kile wanachotaka.’

Bwana Cuttrack huenda akafungwa jela kwa miaka 3. Mwanaharakati wa kisiasa na anaaminikuwa kukamatwa kwake huenda kunahusishwa na msimamo wake unaopinga serikali.

Ni madai ambayo polisi wamekanusha vikali.

Kamishna wa polisi eneo la Odisha, anasema anajitahidi kukomesha usambaaji wa uvumi chanzo cha taarifa za uwongo kwenye mitandao ya kijamii.

The post Raia mmoja wa Marekani aeleza “Nimekamatwa kwa kudanganya nina corona kwenye Facebook” appeared first on Bongo5.com.