Ecuador imesema polisi wameondoa karibu miili 800 katika wiki za karibuni kutoka katika makazi mjini Guayaquil, sehemu iliyoathiriwa kwa kiasi kikubwa na mlipuko wa virusi vya corona, baada ya ugonjwa huo kuzidi uwezo wa huduma za dharura, hospitali na kampuni za mazishi.

Wafanyakazi katika vyumba vya kuhifadhia maiti katika mji huo wa pwani wamekuwa wakishindwa kukabiliana na vifo, huku wakazi wakituma video katika mitandao ya kijamii zinazoonyesha miili iliyotelekezwa mitaani


Ecuador ambayo kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya corona kilibainika Februari 29 kwa sasa ina maambukizi 7,500 na kwamba vifo ambavyo vinahusishwa na virusi vya corona vinakadiriwa kuwa kati ya 2,500 na 3,500.