Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 08/04/2020 ofisini kwake jijini Dodoma ambapo ameitaka kampuni ya Benchmark 360 Ltd ambao ni waandaji wa mashindano ya kutafuta vipaji vya muziki ya Bongo Star Search (BSS) kumlipa mshindi wa mashindano ya BSS 2019 Ndg. Meshack Fukuta ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo.

Meshack aliibuka mshindi kwenye mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo kampuni ya Benchmark walitakiwa kumlipa mshindi kiasi cha shilingi milioni 50 ambapo kati ya hizo, milioni 30 ni kwa ajili ya usimamizi na promotion na milioni 20 alipaswa kukabidhiwa mkononi. Hata hivyo hadi kufikia leo Benchmark hawajamlipa Ndg. Meshack jambo lililopelekea kuleta malalamiko yake kwa Naibu Waziri.

Naibu Waziri amesisitiza kuwa endapo kampuni ya Benchmark haitokamilisha malipo hayo ndani ya mwezi mmoja basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuyafungia mashindano hayo.

View this post on Instagram

#Bongo5Updates: Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 08/04/2020 ofisini kwake jijini Dodoma ambapo ameitaka kampuni ya Benchmark 360 Ltd ambao ni waandaji wa mashindano ya kutafuta vipaji vya muziki ya Bongo Star Search (BSS) kumlipa mshindi wa mashindano ya BSS 2019 Ndg. Meshack Fukuta ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo. Meshack aliibuka mshindi kwenye mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo kampuni ya Benchmark walitakiwa kumlipa mshindi kiasi cha shilingi milioni 50 ambapo kati ya hizo, milioni 30 ni kwa ajili ya usimamizi na promotion na milioni 20 alipaswa kukabidhiwa mkononi. Hata hivyo hadi kufikia leo Benchmark hawajamlipa Ndg. Meshack jambo lililopelekea kuleta malalamiko yake kwa Naibu Waziri. Naibu Waziri amesisitiza kuwa endapo kampuni ya Benchmark haitokamilisha malipo hayo ndani ya mwezi mmoja basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuyafungia mashindano hayo.

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

By Ally Juma.

The post Naibu Waziri Shonza aitaka BSS kumlipa mshindi wa shindano hilo pesa zake ndani mwezi mmoja appeared first on Bongo5.com.