Na Amiri kilagalila,Njombe
Mzee Arusha Nziku (75) mkazi wa wilaya ya Wanging’ombe mkaoni Njombe,amekutwa amefariki nyumbani kwake huku akiwa amefungwa kamba ndani ya nyumba yake kuonyesha amejinyonga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema waliotekeleza mauaji hayo walitumia kamba kumfunga na kuonyesha kama amejinyonga.

“Ni mzee ambaye amekufa akiwa nyumbani kwake na hawa wauaji walichokifanya ni kwamba baada ya kumuua wakamfanya kama amejinyonga,ile kamba wameifunga lakini kwa ufupi wa lile jengo na urefu wa ile kamba inaonyesha kifo ni cha mashaka”alisema Hamis Issa

Amesema mpaka sasa jeshi la polisi limeingia kazini kuhakikisha ni kitu gani kilicho sababisha kifo cha mzee huyo.