Vifo vya watu waliofariki kwa kusombwa na maji wilayani Kiteto mkoani Manyara, vimefika nane kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo.

Mvua kubwa yasababisha vifo Manyara

Mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na mazao mashambani na kupelekea kutishia uhai wa binadamu.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Eatv, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, wakati akiwa katika zoezi la kuokoa mwili wa mwananchi mmoja aliyefariki kwa kusombwa na maji katika daraja la Chem chem.

Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kuchukua tahadhari pindi wanapovuka sehemu zenye maji mengi hasa katika kipindi hiki cha mvua nyingi.

The post Mvua yasababisha uharibifu mkubwa Manyara, 8 wafariki kwa kusombwa na maji appeared first on Bongo5.com.