Msanii wa muziki Muumini Mwijuma amefunguka jinsi alivyopata shinda kuonana na kuzungumza na Diamond toka alionyoonana naye mara ya mwisho mwaka 2010 Temeke jijini Dar es salaam. Muimbaji huyo amedai kukutana na Rais Magufuli ni rahisi kuliko kukutana na Rais huyo wa WCB.

“Kuna wakati nilipiga simu akapokea mama yake akanimbia kama unashida naye ongea na mimi, kila kitu malizana na mimi. Nilijisikia unyonge kwa sababu yeye sio msanii mwenzangu, nilitaka niongee na mwanamuziki mwenzangu. Natamani kufanya naye kazi lakini toka siku hiyo sijawahi onana naye tena, yaani hata ukiwaambia wale watu wake  nitakuwa rahisi kukutana na Mhe Rais Magufuli kuliko kukutana na Diamond”

The post Muumini: Wanaringa, kukutana na Rais Magufuli ni rahisi kuliko kukutana na Diamond, sisi hatukuwa hivyo (Video) appeared first on Bongo5.com.