SALVATORY NTANDU
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Joseph Masanja(58)  mlinzi wa mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Shinyanga kwa tuhuma ya kumbaka Mwanafunzi mwenye Umri wa Miaka 10 wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi.

Tukio hilo lilitokea tarehe 21 machi mwaka huu ambapo mtuhumiwa alimdanganya binti huyo aliyekuwa na mwanzake mwenye umri wa miaka saba kwenda katika eneo lake la kazi kwa madai ya kuwapatia fedha za kununua ndala.

Kwa mujibu wa kamanda wa Jeshi la pilisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema kuwa,mtuhumiwa alikamatwa baada ya binti hiyo kutoka katika eneo la kazi majira ya saa kumi na moja jioni.

“Ilikuwa saa nane mchana siku ya Jumamosi,mabinti hao walifika mahakamani, Joseph aliagiza binti wa miaka saba kubakia getini na kisha yeye kuingia ndani binti huyu na kumbaka katika  mmoja ya chumba cha  ofisi katika eneo la Mahakahama”alisema Magiligimba.

Aidha Magiligimba alifafanua,Joseph baada ya kutekeleza tukio hilo alimwamuru binti  huyo kuondoka eneo la tukio kwa kupitia geti lingine ambapo mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Mwenge aliyefamika kwa jina mmoja la Leticia alipomkamata binti huyo na alimhoji kuwa ametokea wapi ndipo alipokili alikuwa akifanya mapenzi na mlizi huyo.

“Kuna Afisa wa polisi alimwona binti wa miaka saba aliyekaa getini muda mrefu,alipomhoji kwanini amekaa kwa muda mrefu katika eneo hilo alijibiwa kuwa anamsubiri mwenzake tangu majira ya saa 8 mchana alipoingia ndani na Mlinzi huyo hajatoka”aliongeza Magiligimba.

Magiligimba aliendelea kusema kuwa,Askari huyo alimchukua binti huyo na kuingia nae ndani ya eneo la mahakama na kukutana na mwalimu aliyemkamata binti wa miaka 10 wakati akipitishwa geti la pili na joseph,ndipo walipoamua kutoa taarifa kwa wazazi wa mabinti hao.

Aidha alisema kuwa,baada ya mabinti hao kufikishwa polisi wazazi wao walifika na kupewa kibari cha kwenda hospitali kwaajili ya vipimo na vipimo vilibaini kuwa binti wa miaka 10 ameingiliwa(kubakwa)

Hata hivyo Magiligimba alisema,baada ya joseph kutekeleza tukio ,alikimbia kusikojulikana hadi alipokuja kukamatwa na jeshi la polisi na alipohojiwa alikiri kumbaka mwanafunzi huyo,na upepelezi wa tukio utakapokamilika atafikishwa mahakani kujibu tuhuma hizo.

Mwisho.