Mtoto wa miaka mitatu, Adam Kaliambe amepoteza maisha baada ya kutumbukia katika mtaro mkubwa wa maji machafu akivuka kuelekea dukani mkoani Tanga.

Picha si halisi
Kwa mujibu wa Baba mzazi wa marehemu, Emanuel Kaliambe, ni kwamba tukio hilo lilitokea majira ya saa moja jioni katika mtaa wa Mjimwema Magomeni Jiji la Tanga.
Kaliambe amesema siku ya tukio yeye na mtoto huyo walienda nyumbani kwa mdogo wake na hapo mtoto huyo aliomba shilingi mia ya kununua pipi na baada ya kupewa alitoka na kuelekea dukani ambako hakurudi tena.
By Ally Juma.
The post Mtoto wa miaka 3 adumbukia kwenye mtaro na kupoteza maisha wakati akijaribu kuruka akielekea dukani – Video appeared first on Bongo5.com.