Msanii wa Kings Music K2ga, Amuandikia Alikiba waraka mrefu baada ya wenzake kuondoka
Ikiwa imepita takribani wiki moja tangu wasanii Killy na Cheed kutangaza kujitoa kwenye lebo ya Kings Music Records, msanii aliyebakia ambaye walitambulishwa pamoja ndani ya kundi hilo amesema bado yupoyupo sana kwa Alikiba.
Msanii K2ga upande wa kushoto akiwa na Alikiba
Msanii huyo ambaye ni K2ga amesema amehuzunika na anapata wakati mgumu sana baada ya wenzake kuondoka, huku mashabiki wamekuwa wakimuuliza hatma yake ndani ya Kings Music.
Akitoa maelezo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram K2ga ameandika kuwa “Ndugu mashabiki na wapenzi wangu, nimepata meseji nyingi na simu nyingi pamoja na comment zakutosha sana kutoka kwenu wote mkiulizia juu ya hatima yangu, najua mmehuzunika hata mimi pia nimehuzunika, nimepata wakati mgumu mno kwa muda wa wiki moja sasa“.
“Hatimae kwa utashi wangu niloyopewa na Muumba na kwa unyenyekevu mbele yenu mashabiki nimeamua kubaki Kings Music Records, nampenda sana Alikiba, nawahusudu mashabiki zangu. Ni yeye alinitambulisha kwenu akanifungulia dunia kwa moyo wake wa upendo mmenipokea kwa mikono miwili, naomba sana ndugu zangu muendelee kubaki na mimi” ameongeza