Msanii wa muziki wa bongo Fleva Msamii ameongea na kuonyeshwa kukerwa na amneno ambayo Mwijaku aliyazungumza kuhusu yeye. Msanii ameongeza kuwa mara nyingi vitu anavyoongea Mwijaku hajui huwa anasababisha matatizo kiasi gani kwenye familia za watu.

Msamii amemshauri Mwijaku kuacha kuzungumzia maisha ya watu kwani hakuna mtu anayemzungumzia Mwijaku sasa kwanini yeye azungumzie watu.

“Mfano anapomzungumzia msanii kama Q Chillah kuwa walimsaidia kutoka kwenye madawa kwahiyo anafurahia kuona msanii anapotea au anapomponda Mzee Yusuf baada ya kusema anarejea kweney muziki alipokuwa anapata shida yeye alienda kumsaidi?, Mimi namjua Mwijaku tumeishi wote THT na ndio nimempokea anapata wapi nguvu za kuzungumzia mapenzi wakati yupo kwenye wimbo la kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume.”

“Aliletwa na marehem Ruge kama mtu wa Marketing nashangaa kaingia mpaka huku sitakashangaa nikimuona anataka kuimba, halafu mimi namjua kama Mwemba na sio Mwijaku”

The post Msamy “Mwijaku aliletwa THT na marehmu Ruge kama mtu wa marketing eti sasa hivi msanii, Tunamjua anatumia dawa za kuongeza nguvu za kiume ” – Video appeared first on Bongo5.com.