Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mkali wa ngoma ya #babygirl @msamibaby amefunguka mazito sana kuhusu historia ya maisha yake hadi kuonana na marehem Ruge na kumpeleka THT.


Mbali na hilo @msamibaby ameeleza jinsi alivyofanya kazi na @diamondplatnumz na kusema kuwa wasanii wenzake walikuwa wanamkatisha tamaa kuwa hajui ila @diamondplatnumz ndio msanii wa kwanza aliyemwambia anaweza na anajua hadi walitaka kufanya wimbo wa Soundtrack lakini @diamondplatnumz alikuwa bize sana.

Msamii pia ameeleza jinsi alivyotetereka kimuziki baada ya marehemu Ruge kutangulia mbele ya haki “Ruge kwangu alikuwa baba alikuwa kaka alikuwa mjomba yani kila kitu, aliniamini mimi hadi akaniachia password za laptop yake alikuwa anaishi na sisi kama watoto wake akikuta unakula na yeye ataonja, hadi leo Email zake sijafuta meseji zake hadi namba yake naiangaliaga tu”

By Ally Juma.

The post Msami “Diamond ndio msanii wa kwanza kuniambia naweza kuimba, Nilikuwa mwizi Ruge akaniokoa kanipeleka THT alikuwa kama baba yangu” – Video appeared first on Bongo5.com.