Serikali wilayani Hai imefanya msako maalum katika maduka ya yanayouza sukari mjini Boma’ngombe na kukamata Wafanyabiashara 7 waliokiuka maagizo ya serikali kwa kupandisha Bei kutoka sh 2700 hadi 3500.
Mkuu wa wilaya hiyo @lengai_ole_sabaya aliamuru kukamatwa kwa watu hao na kufungwa kwa maduka yao kwa kukiuka maelekezo ya serikali na kutumia Ugonjwa wa Corona na mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwanyanyasa wananchi.
Ukaguzi huo umefanyika baada ya Mkuu wa wilaya kutuma watu kwa siku tatu mfululizo kujua mienendo ya biashara hiyo wilayani hapo.
The post Msako Wilaya ya Hai, Wafanyabiashara 7 wakamatwa kwa kukiuka bei elekezi ya Sukari- Video appeared first on Bongo5.com.