Jose Mourinho ameingia matatani na mabosi zake wa Tottenham baada kuruhusu kuanza kwa mazoezi yeye na wachezaji wake tena bila kufuata taratibu za kuwa mbalimbali ili kuepuka virusi vya Corona.
Kocha huyo wa Tottenham, Mourinho amepigwa picha hapo jana siku ya Jumanne akiwa na wachezaji watatu ambao wamevalia jezi za mazoei za Spurs.
Wachezaji hao wakiwa ni Davinson Sanchez, Tanguy Ndombele na Ryan Sessegnon, ambapo vipande vya video vimeanza kuonekana katika mitandao ya kijami, zikimuonyesha Sessegnon na Sanchez wakiwa wamesogeleana kwa karibu kabisa huku Mourinho akipigwa picha akiwa na Ndombele pamoja na watu wengine wawili wakifanya mazoezi.
Kwa mujibu wa ushauri wa serikali juu ya virusi vya Corona, ni kuwa kila mtu angalau kuwa umbali wa mita mbili lakini ni tofauti na video zilizorikodiwa wakati wachezaji hao wakifanya mazoezi wakionekana kuwa wamekaribiana.
Uongozi wa Spurs umeonekana kutofurahishwa na kitendo hicho cha Mourinho kuandaa mazoezi hayo. Msemaji wa klabu ya Tottenham amesema “Wachezaji wetu wote wamekumbushwa kuheshimu utaratibu wa kuwa mbalimbali wakati wa mazoezi. Tunaendelea kusisita ujumbe huu.”
The post Mourinho alikoroga, ni baada ya kuwaingiza wachezaji mazoezini kipindi hiki cha Virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.