Meneja Diamond na Mkubwa na Wanae, Mkubwa Fulla amefunguka kuizungumzia kauli yake ambayo aliitoa hivi karibuni kwa aliyekuwa msanii wa Yamoto Band Mbosso baada ya kupost picha za nyumba ambazo walijengewa na meneja huyo.

Katika ujumbe wa Mbosso alidai amejenga nyumba hiyo kwaajili ya wazazi wake wakati nyumba hizo walijengewa na Mkubwa Fella wakati wanafanya kazi chini ya Yamoto Band.

Baada ya post hiyo ya Mbosso, Fella aliandika ujumbe “Ni vizuri kuweka kumbukumbu na sio historia” kauli ambayo imetafsiriwa tofauti na baadhi ya watu.

Bongo5TV imefanya mahojiano na Mkubwa Fella kuhusiana na ishu hiyo.

The post Mkubwa Fella amkumbusha jambo Mbosso “Tujifunze kusema asante” (Video) appeared first on Bongo5.com.