Msanii mkongwe wa muziki wa mduara Bob Haisa ambaye alitamba na kibao cha MBELEKO amerudi rasmi kwenye muziki baada ya kukaa kimya kwa takribani miaka 8. Akieleza ameseam kuwa katika miaka hiyo 8 alijiingiza kwenye biashara ya kuokota makopo baada ya maisha kuwa magumu.

“Nakumbuka ilikuwa Tabata tunafanya video ya wimbo, mimi niliigiza kama muokota makopo lakini baada ya video kuisha yale makopo tukakosa sehemu ya kuyatupa maana palikuwa pasafi”

Bob Haisa ameongeza kuwa “Wakati tunatafuta sehemu ya kwenda kuyatupa kuna muokota makopo akayanunua na kunipa elfu mbili hiyo nahisi nilijipa laana pale” “Baada ya kurudi Mwanza nikakaa sina hata senti nikajiuliza nifanye kazi gani ndio nikakumbuka makopo maana yalikuwa yamezagaa mtaani, hapo ndio nikazama mazima”

Mbali na hilo @bobhaisatz ameongeza kuwa anatamani sana kufanya kazi na msanii yeyote wa WCB lakini pia @harmonize_tz @barnabaclassic @officialnandy pamoja @mauasama

By Ally Juma.

The post Mkongwe wa muziki wa mduara Bob Haisa, Asimulia alivyofanya kiki ya kuokota makopo na kupata laana ya kuwa muokota makopo maarufu – Video appeared first on Bongo5.com.