Muigizaji huyo maarufu kutoka tasnia ya filamu za Kihindi (Bollywood) aliyetamba katika filamu za ‘Slumdog Millionaire’ na ‘Jurassic World’ amefariki leo asubuhi akiwa na miaka 53.

Mwaka 2018, alitangaza kuwa na saratani katika mfumo wa tezi zinazotengeneza homoni (Endocrine Tumour). Tangu jana amekuwa kwenye Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU) hospitali kutokana na bakteria kwenye utumbo ‘Colon Infection’.

Mwaka 2013, alishinda tuzo ya Kitaifa ya Filamu za India kutokana na filamu ya Paan Singh Tomar. Filamu nyingine alizotamba nazo ni Lunchbox, The Namesake, New York, I Love You na Hindi Medium. Ya mwisho, Angrezi Medium imetoka mwezi uliopita.

Khan amezikwa katika makaburi ya Versova Kabristan huko Mumbai muda mfupi baada ya taarifa zake za kifo kutolewa. Familia, ndugu na marafiki wa karibu ndio wamehudhuria.

The post Mfahamu Irrfan Khan, Mcheza filamu maarufu India aliyepoteza maisha appeared first on Bongo5.com.