Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 32, amekanusha kwa kupitia mitandao ya kijamii ripoti kuwa ana mpango wa kuhamia klabu ya Inter Milan. (Instagram)

Lionel Messi

Klabu ya Everton inaamini kuwa mustakabali wa kucheza chini ya kocha Carlo Ancelotti unaweza kumshawishi kiungo wa Aston Villa Jack Grealish, 24, kuhamia klabu hiyo. (Football Insider)

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelloti

Beki wa zamani wa Chelsea Frank Leboeuf amemuonya kocha wa klabu hiyo Frank Lampard dhidi ya kumsajili kiungo wa Brazil Philippe Coutinho, 27, kutoka Barcelona. (ESPN)

Klabu ya AS Roma imempa nafasi kiungo wa Chelsea Pedro, 32, kujiunga na kikosi chake mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wa mchezaji huyo na Chelsea utakuwa unafikia kikomo. (Mirror)

Pedro

Beki wa pembeni wa Manchester City na Ureno Joao Cancelo, 25, anatakiwa na klabu ya Barcelona katika makubaliano ambayo Barceola pia itawapa City beki raia wa Ureno – Nelson Semedo, 26. (Telegraph, subscription required)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema anamipango “miwili ama mitatu tofauti” juu ya dirisha la usajili lijalo. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Rivaldo, 47, amemshauri mshambuliaji nyota wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 21, kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu. (Betfair)

Mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe

Arsenal na Manchester United wapo katika mbio za kutaka kumsajili kiungo wa Bayern Munich na Ufaransa Corentin Tolisso, 25. (Foot Mercato, in French)

Kipa wa zamani wa Nigeria Dosu Joseph anasema mshambuliaji Odion Ighalo, 30, amefanya vya kutosha ili kusajiliwa moja kwa moja na Manchester United Shanghai Shenhua.. (Goal.com)

Mshambuliaji wa Man United Odion Igalo

Kiungo wa Bayer Leverkusen Kai Havertz, 21, anataka kubaki Ujerumani na kujiunga na vigogo wan chi hiyo klabu ya Bayern Munich pindi dirisha la usajili llitakapofunguliwa. (Sky Germany)

The post Messi akanusha jambo hili, Kylian Mbappe ashauriwa kujiunga na Real Madrid appeared first on Bongo5.com.