Wakati Ligi Kuu soka Tanzania Bara imesimama kwa muda ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali katika kuhakikisha inapambana na kuenea kwa ugonjwa wa Virusi vya Corona. Mchambuzi wetu wa kabumbu na anayekuja kwa kasi nchini, Abbas Pira amezungumzia mecho bora kwa upande wake iliyowahi kuchezwa msimu huu wa mwaka 2019/20.
Pira ameutaja mchezo wa #YangaSC dhidi ya #SimbaSC kama ‘game’ bora zaidi kwa upande wake hasa kutokana na umahiri, uweledi na ubunifu mkubwa uliyofanya na wachezaji wenyewe pamoja na benchi zima la ufundi kwa timu zote mbili. Katika mchezo huo Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC iliweza kuibuka na ushindi mwembamba wa goli 1 – 0 dhidi ya mtani wake wa jadi na Bingwa mtetezi Simba SC. Goli hilo lilifungwa na Mghana, Bernard Morrison.
The post MECHI BORA YA MSIMU: Mchambuzi Abbas Pira aichambua ‘Game’ bora ya ligi kwa upande wake (+Video) appeared first on Bongo5.com.