Mbunge wa Jimbo la Rombo, Joseph Selasini, leo Aprili 28, 2020 ametangaza rasmi kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi baada ya kumalizika kwa vikao vya  Bunge.

Jana, Selasini alidai kutengwa na wabunge wenzake wa chama chake cha CHADEMA ikiwemo  kuondolewa bila kupewa taarifa kwenye 'Group la WhatsApp' la Wabunge wa chama hicho  ambalo pia yumo Mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe