Mataifa yaliyoathiriwa vibaya na virusi vya corona barani Ulaya yanajitayarisha kuanza kufungua shughuli za umma huku mji wa New York nchini Marekani ukitangaza kupiga hatua muhimu kukabiliana na virusi vya va corona.
Bara la Ulaya limeshuhudia dalili za kutia moyo baada ya Italia, Uhispania, Ufaransa na Uingereza kuripoti idadi ndogo ya vifo na maambukizi ya virusi vya corona siku ya Jumapili.
Hadi sasa bara hilo ndiyo limerikodi karibu theluthi mbili ya vifo 165,000 vya ugonjwa wa COVID-19 vilivyotokea duniani wakati maambukizi ya virusi vya corona yamepindukia visa milioni 2 na laki 3 leo Jumatatu
Ushahidi wa kitaalaum umethibitisha hatua za kujitenga na vizuizi vilivyowekwa vinapunguza kusambaa kwa virusi vya corona na hali hiyo imechochea mipango ya mataifa mengi kuanza kulegeza marufuku zilizowekwa na kufungua tena shughuli za kawaida.
Uhispania moja ya taifa lililoathiriwa vibaya limerefusha viuzizi vyake kwa nchi nzima lakini imesema itaanza leo kuwaruhusu watoto kutoka nje.
Nchi hiyo ilitangaza vifo 410 siku ya Jumapili, ambayo ni idadi ndogo kabisa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliopita na maafisa wa afya wamesema rikiodi hiyo inatoa matumaini.
Mamlaka nchini humo wameanza kuyafunga maeneo kadhaa yaliyotengezwa haraka kukabiliana na wimbi la virusi vya corona ikiwemo eneo la kuhifadhi maiti katika uwanja wa michezo ya kwenye barafu mjini Madrid.
Mataifa mengine pia yatafungua shughuli za umma
Uswisi, Denmark na Finland zote zimetangaza kuyafungua tena maduka pamoja na shule zote kwenye mataifa hayo.
Ujerumani leo itaruhusu baadhi ya maduka kufunguliwa tena baada ya kutangaza kuwa imefanikiwa kudhibiti viruis vya corona huku Italia yenyewe ikijikongoja kuchukua hatua za kufungua tena shughuli za kawaida.
Iran, taifa linalokabiliwa na mlipuko mbaya kabisa wa virusi vya kaitka eneo la mashirki ya kati siku ya Jumamosi ilianza kuruhusu kufunguliwa biashara zilizo kwenye kiwango cha chini cha hatari ya kueneza ugonjwa wa COVID-19.
Nchini Marekani – taifa lenye idadi kubwa ya vifo na maambukizi ya virusi vya corona- gavana wa jimbo la New York Andrew Cuomo amesema mlipuko huo unaelekea kupungua ijapokuwa ametahadharisha bado ni mapema kuanza kujipongeza.
Baada ya wiki kadhaa za mivutano na serikali kuu mjini Washington kuhusu wajibu wake kwenye janga la corona, gavana Cuomo jana alitumia matashi laini na kusifu ushirikiano kati ya serikali kuu na majimbo kwenye mafanikio yanayoonekana.
Hata hivyo Marekani imeshuhudia maandamano ya mwishoni mwa juma ya kupinga vizuizi vilivyowekwa kukabiliana na viruis vya corona.
Waandamanaji katika majimbo ya Colorado, Texas, Maryland, New Hampshire na Ohio walikusanyika kupinga viuzizi hivyo wakisema vinaharibu uchumi na kusabaisha ukosefu wa ajira.
Chanzo DW.
The post Mataifa ya Ulaya kuanza kufungua shughuli za umma appeared first on Bongo5.com.