Majimbo matatu nchini Marekani yameruhusu baadhi ya maduka kufunguliwa tena baada ya hatua zilizowekwa za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.
 
Saluni za wanaume na wanawake sasa zinaweza kufunguliwa tena katika majimbo ya Georgia Oklahoma huku Alaska ikiondoa masharti iliyokuwa imewekea migahawa.

Vifo vinavyotokana na corona vimeendelea kuongezeka Marekani ambapo hadi asubuhi hii wamefariki Watu 54,265.

Marekani inaongoza kwa vifo vingi Duniani pia kwa visa ambapo leo vimefikia 960,896 na wamepona 118,162,

Rais wa nchi hiyo Donald  Trump amekabiliwa na ukosoaji mkubwa baada ya kupendeza kuwachoma sindano ya kemikali za kuua vimelea au za usafi wagonjwa wa corona

Kauli zake zimekua zikilaaniwa na madaktari pamoja na watengenezaji wa bidhaa wanaozitaja kuwa ni za hatari. 

Kemikali za kuua vijidudu au vimelea zinaua na zinaweza kuwa sumu zikiingizwa katika mwili wa binadamu , na hata matumizi yake ya nje ya mwili yanaweza kuwa hatari kwa ngozi, macho na mfumo wa kupumua.