Majimbo matatu nchini Marekani yameruhusu baadhi ya maduka kufunguliwa tena baada ya hatua zilizowekwa za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona, huku idadi ya vifo nchini humo ikizidi watu 51,000.

Los Angeles, California, USA early morning downtown cityscape.

Saluni za wanaume na wanawake sasa zinaweza kufunguliwa tena katika majimbo ya Georgia Oklahoma huku Alaska ikiondoa masharti iliyokuwa imewekea migahawa.

Ijumaa rais Donald Trump aliondoka mapema kuliko ilivyo kawaida wakati otuba yake ya kawaida kuhusu maendeleo ya hali ya janga la corona, akakataa kupokea maswali ya waandishi wa habari.

Rais Trump amekabiliwa na ukosoaji mkubwa baada ya kupendeza kuwachoma sindano ya kemikali za kuua vimelea au za usafi wagonjwa wa corona inaweza kuwa ni jambo la manufaa.

Kauli zake zimekua zikilaaniwa na madaktari pamoja na watengenezaji wa bidhaa wanaozitaja kuwa ni za hatari. Kemikali za kuua vijidudu au vimelea zinaua na zinaweza kuwa sumu zikiingizwa katika mwili wa binadamu , na hata matumizi yake ya nje ya mwili yanaweza kuwa hatari kwa ngozi, macho na mfumo wa kupumua.

Bwana Trump alisema siku ya Ijumaa kuwa kauli-alizozitoa katika mkutano wa wanahabari siku moja kabla zilikuwa za vichekesho na muktadha wake ulipotoshwa.

Je ni nini kinachoendelea katika majimbo hayo matatu?

Wateja wanaotembelea biashara mpya zilizofunguliwa katika majimbo ya Georgia, Oklahoma na Alaska watatarajiwa kuendelea kuheshimu hatua za kutosogeleana .

Lakini baadhi ya miji na maeneo wameamua kuendelea kutekeleza hatua yao ya kukaa nyumbani.

Barber shop in AtlantaBarber shops opened in Georgia on Friday

Katika jimbo la Georgia, ambalo lina moja ya ratiba ya haraka sana ya kufungua shughuli nchini humo ,saluni za wanaume na wanawake, za kutengeneza kucha , tatuu, na biashara nyingine za mapodozi zitaruhusiwa kufungua shughuli zake.

Siku ya Jumatatu migahawa ya chakula na kumbi za michezo zitaruhusiwa kufunguliwa tena.

Huku kukiwa na madai ya ukosefu wa ajira kwa watu milioni 26-au takribani 15% ya watu wa Marekani – tangu katikati mwa mwezi Machi, majimbo menfufua biashara zilizositishwa kutokana na janga la corona.

Lakini wataalamu wa afya wameonya kuwa hatua hizo huenda zikawa zimechukuliwa mapema, huku kukiwa na hofu kwamba zinaweza kusababisha wimbi jingine la maambukizi.

Baada ya kukosolewa na Trump,Gavana wa jimbo la Georgia Brian Kemp amri kali za usafi na watu kutosogeleana kuhusu kuhusu migahawa.

Je ni yapi zaidi yaliotokea Ijumaa?

Katika hotuba ya White House iliyodumu kwa muda wa dakika 20,Bwana Trump aliwaomba watu kuendelea kufuata sheria zinazohusu kutotengamana kwa watu katika jamiina kutumia barakoa.

Pia Ijumaa, Bwana Trump pia alisaini muswada wa thamani ya bilioni 484 (Pauni Bilioni 391) za kuchochea uchumi , akisema kuwa anataka “kuharakisha nafuu ya kiuchumi kwa ajili ya raia wetu”.

Ni msaada wan ne wa Covid-19 ikupima virusi, hospitali na mpango wa mikopo ya biashara ndogondogo.

Je, Marekani ni ipi idadi ya Marekani ?

Marekani ina idadi kubwa zaidi ya vifo na visa corona kuliko nchi nyingine duniani- zaidi ya vifo 50,000 na visa 890,000 vimethibitishwa.

Lakini nchi za Ulaya, mkiwemo Uhispania na Italia, zimerekodi vya juu zaidi ikilinganishwa na idadi ya watu kuliko Marekani ambayo ina jumla ya watu milioni 330.

Kupanda haraka kwa hivi karibuni kwa idadi ya vifo kwa sehemu kubwa ni kujumuishwa kwa “labda” kwa idadi ya vifo – Tarehe 14 Aprili, Kituo cha Marekani udhibiti wa magonjwa kilisema hesabu ya visa vya maambukizi itajumuisha visa vilivyothibitishwa na visa vinavyoshukiwa pamoja na vifo kwa pamoja.

Kifo kinachoshukiwa kuwa kimetokana na Covid-19 ni mojawapo ya vile vinavyodhaniwa kimatibabu lakini bado havijathibitshwa.

Pia ni muhimu kutambua kuwa visa vingi ambavyo muathiriwa hupati madhara vinasalia kutotangazwa, kwa hiyo kiwango visa vya vifovilivyothibitishwa sio sawa na kiwango cha vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa corona kwa ujumla.

Juhudi za kupima ni muhimu katika kutafuta visa halisi vya vifo na jinsi ugonjwa unavyosambaa. Makamu rais Mike Pence, ambaye ni kiongozi wa kikosi kazi cha kupambana na Covid-19, alisema kuwa Marekani imewapima watu 4.9 hadi sasa, na kwamba serikali inashirikiana na magavana kupanua zaidi upimaji wa virusi wa virusi vya corona.

The post Majibo haya matatu Marekani yaanza kufungulia watu licha ya vifo vya Corona kuongezeka na kuwa zaidi ya elfu 51 appeared first on Bongo5.com.