Takriban mabaharia 34 waliokuwa kwenye meli ya safari za kitalii iliyotia nanga katika mji wa Nagasaki nchini Japan wamegundulika kuwa na virusi vya Corona kwa mujibu wa mamlaka za Japan.

Msemaji mkuu wa serikali Yoshihide Suga amesema kuwa meli ya Costa Atlantica iliwasili kwa mara ya kwanza Nagasaki mnamo mwezi Januari kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati ikiwa imewabeba mabaharia 600.

Mwishoni mwa wiki iliyopita wasimamizi wa meli hiyo waliwasiliana na mamlaka kutaka msaada wa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya watu kadhaa waliokuwa wakishukiwa kuwa na virusi hivyo. Mabaharia wote wako ndani ya meli ikiwemo waliokutwa na virusi.

The post Mabaharia 34 wakutwa na Virusi vya Corona, Japan appeared first on Bongo5.com.