Kwa mujibu wa Jarida la Telegraph limeripoti kuwa Ligi Kuu ya England inaweza kukamilisha msimu wake katika muda wa wiki tano tu, Inatarajiwa kuwa timu za EPL zinaweza kucheza karibu michezo miwili kwa wiki kwa zaidi ya siku 35 kumaliza msimu wa 2019-20.
Imependekezwa pia uwanja wa Wembley ndio utatumika kama “neutral-ground” na kwa siku zaidi ya michezo minne ifanyike. Vilabu vinataka kumaliza msimu ili kuepuka athara kutoka kwenye kampuni za Televisheni – ambapo bila hivyo vilabu vinaweza kulipa fedha nyingi.
Chanzo kimeeleza kuwa ” Hadi Kufikia mwezi Juni au Julai vilabu vitakuwa vikicheza michezo yao bila mshabiki ingawa itakuwa ikiruka live kupitia runinga” Itabidi kucheza michezo minne kwa siku katika uwanja wa Wembley ili kuimaliza kwani vilabu vingine vina michezo takribani tisa watafanya hivyo ili kumaliza msimu”
Hadi sasa, hakuna tarehe maalumu ya kurudi iliyowekwa ambayo itakuwa rasmu kwa kureje Ligi Kuu, ingawa katika taifa hilo bado watu hawatakiwa kutoka nje kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
By Ally Juma.
The post Ligi ya Uingereza sasa kurejea na kuchezwa bila mashabiki, Uwanja huu wapendekezwa kutumika kwa minne kwa siku appeared first on Bongo5.com.