Kuingia Hospitali Ya Bugando Kuanzia Leo Ni Lazima Uvae Barakoa (Mask)
Kuanzia leo Aprili 24, 2020, mtu yeyote yule, wakiwemo wagonjwa ama ndugu za wagonjwa atakayeingia katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, atatakiwa kuvaa barakoa na kuirejesha getini kabla ya kutoka, ikiwa ni hatua ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.