Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un yuko katika hali nzuri ya kiafya  kwa mujibu wa Moon Chung In, mmoja wa washauri wa usalama wa rais wa Korea Kusini Moon Jae-in.

Chung amesema kiongozi huyo wa Korea Kaskazini amekuwa katika mji wa Wonsana tangu april 13 na hajafanya ziara nyingi kama ilivyo ada yake, na kuwa yuko salama kinyume na uvumi kuwa amefariki.

Wakati huo picha za satelaiti zimeonyesha treni inayodhaniwa kuwa ni ya kiongozi huyo ikiwa imeegeshwa kwenye makazi yake yaliyoko pwani ya mashariki mwa nchi hiyo tangu wiki iliyopita.

Picha hizo za satelaiti zilizochapishwa na tovuti ya 38 North ambayo ni maalumu kwa masomo kuhusu Korea Kaskazini, hata hivyo hazielezi chochote kuhusu matatizo ya kiafya ya Kim Jon-un, lakini zinaendeleza taarifa za kiintelijensia za Korea Kusini kwamba Kim yuko nje ya mji mkuu, Pyongyang.

Uvumi kuhusu hali yake ya kiafya, kwa sehemu kubwa umesababishwa na kutoonekana kwake hadharani kwa kipindi kirefu.

Credit:RFI