Korea Kaskazini imefyatua makombora kadhaa katika bahari yake ya mashariki hapo jana. Hayo ni kwa mujibu wa jeshi la Korea Kusini ambalo limeongeza kwamba makombora hayo yanaaminiwa kuwa ni ya masafa mafupi.

Korea Kusini imesema makombora hayo maalumu kwa ajili ya kushambulia meli yalifyatuliwa kutoka mji wa pwani wa Munchon na kuruka umbali wa kilomita 150 kabla ya kutuwa baharini.

Korea Kaskazini ilifyatua makombora kadhaa ya masafa mafupi mnamo mwezi Machi huku mazungumzo yake na Marekani kuhusu silaha za nyuklia yakiwa yamekwama.

Makombora hayo yamefyatuliwa jana ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Korea Kaskazini Kim Il-sung na uchaguzi mkuu wa Korea Kusini.

The post Korea Kaskazini yafyatua makombora, yadaiwa kuruka umbali wa kilomita 150 appeared first on Bongo5.com.