Kwa mara ya kwanza msanii wa muziki wa Bongo Fleva Killy amefunguka  kama mmoja kati ya waliojiengua kwenye lebo ya Kings Music inayosimamiwa na Alikiba na ameitaja sababu ilisababisha kuondoka katika lebo hiyo na kuitaj familia yake kama sehemu ya sababu / vishawishi vya wao kufikia maamuzi ya kujiengua Kings music.

Killy ameeleza kuwa maamuzi waliyofikia ni sahihi na yaliyojadiliwa kwa kina kabla ya kufanyika, pia amekanusha story za kushawishiwa na baadhi ya watu wa karibu nje ya familia.

Akiongea katika kituo cha Clouds Media Killy ameongeza kuwa “Niliongea na mama yangu ndio akanishauri na mwenzangu pia aliongea na wazazi wake”

 

By Ally juma.

The post Killy aeleza sababu za kuondoka kwenye lebo ya Kings Music iliyopo chini ya Alikiba “Niliongea na mama yangu ndio amenishauri” – Video appeared first on Bongo5.com.