Waziri wa Afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe amewataka wananchi kuendelea kukaa nyumbani siku ya sikukuu ya Pasaka kufuatia mlipuko wa Virusi vya Corona ili kuepusha kusambaa kwa ugonjwa huo.

View this post on Instagram

#HABARI : KENYA YATANGAZA MARUFUKU WATU KUTOKA NYUMBANI SIKUKUU YA PASAKA . Waziri wa Afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe amewataka wananchi kuendelea kukaa nyumbani siku ya sikukuu ya Pasaka kufuatia mlipuko wa Virusi vya Corona ili kuepusha kusambaa kwa ugonjwa huo. Mutahi Kagwe ameyasema hayo hapo jana Aprili 9 wakati akielezea hali ya ugonjwa huo wa COVID -19 ilivyo kwa sasa nchini Kenya, katika hotuba hiyo Waziri huyo amesema kuwa idadi ya vifo vya wagonjwa Virusi vya Corona vimefikia 7 baada ya hapo jana kuthibitisha kifo cha mtu mmoja. ………………………………………………………………………. ''Wakati huu wa Pasaka, kwasababu hakuna watu wanaokwenda kazini, ni lazima watu wakaye nyumbani, ukiwa kijijini kwako baki hapo hapo usiende sehemu nyingine. #Stayathome . Hakuna mambo ya party, hakuna mambo ya mbuzi eti tunakwenda kula mbuzi sehemu fulani hakuna.'' ………………………………………………………………………. Idadi ya waathirika wa Virusi vya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia 184, baada ya visa vipya vitano kuthibitishwa hii leo, ambapo watatu ni raia wa Kenya na walikuwa wamesafiri kutokea Tanzania na wawili walisafiri kutoka Uingereza na Nchi za Falme za Kiarabu. . WRITTEN BY @fumo255 Video Credit by Kenya Citizen #Bongo5Updates

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

Mutahi Kagwe ameyasema hayo hapo jana Aprili 9 wakati akielezea hali ya ugonjwa huo wa COVID -19 ilivyo kwa sasa nchini Kenya, katika hotuba hiyo Waziri huyo amesema kuwa idadi ya vifo vya wagonjwa Virusi vya Corona vimefikia 7 baada ya hapo jana kuthibitisha kifo cha mtu mmoja.

”Wakati huu wa Pasaka, kwasababu hakuna watu wanaokwenda kazini, ni lazima watu wakaye nyumbani, ukiwa kijijini kwako baki hapo hapo usiende sehemu nyingine. #Stayathome . Hakuna mambo ya party, hakuna mambo ya mbuzi eti tunakwenda kula mbuzi sehemu fulani hakuna.” 

Idadi ya waathirika wa Virusi vya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia 184, baada ya visa vipya vitano kuthibitishwa hii leo, ambapo watatu ni raia wa Kenya na walikuwa wamesafiri kutokea Tanzania na wawili walisafiri kutoka Uingereza na Nchi za Falme za Kiarabu.

The post Kenya yatangaza marufuku watu kutoka nyumbani sikukuu ya Pasaka ”Hakuna mambo ya Party, mbuzi” (+Video) appeared first on Bongo5.com.