Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jana ametangaza kusitishwa kwa safari zote katika maeneo yaliyoathirika na virusi vya corona nchini humo. 

Katika hotuba aliyoitoa , Kenyatta ametaka kusitishwa kwa usafiri wote wa umma kwa njia ya barabara, reli na hata ndege katika kaunti ya Nairobi, Mombasa, Kilifi na Kwale kwa siku ishirini na moja ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona. 

Marufuku hayo yameanza kutekelezwa jana saa moja jioni  huko Nairobi na kuanzia siku ya Jumatano huko Mombasa, Kilifi na Kwale. 

Hapo awali rais Uhuru alitangaza marufuku ya nchi nzima ya kutotoka nje usiku ila maambukizi yanaonekana kuongezeka huku visa vya maambukizi vikifikia 158 baada ya kuripotiwa visa vyengine sita jana. 

Idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo imeongezeka pia na kufikia watu sita.