Wakati Kenya wakiripoti idadi ya wagonjwa walioambukizwa virusi vya Corona kufikia 142, Sudan Kusini imeripoti mgonjwa wa kwanza. Nchi hiyo ni miongoni mwa nchi ambazo zilikuwa hazina maambukizi hadi jana Aprili 4, 2020.

Mgonjwa huyo, mwanamke mwenye miaka 29 aliingia nchini humo akitokea Uholanzi kupitia Ethiopia na uraia wake haujawekwa bayana.

Nchini Tanzania, siku ya jana Wizara ya afya ilitangaza waathirika wa corona visiwani humo imefikia 7 .

Wagonjwa hao wapya wametoka Tanga kwa nyakati tofauti na kuingia Zanzibar kupitia Bandari ya Mkokotoni

The post Kenya wagonjwa wa corona wafikia 142, Sudani Kusini waripoti mgonjwa wa kwanza appeared first on Bongo5.com.