Juventus sasa wanaelekeza nguvu zao kutaka kumsajili mshambuliaji nyota wa Tottenham Harry Kane. (Corriere dello Sport – in Italian)

Harry Kane

Real Madrid wametoka kwenye kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili Harry Kane kutokana na athari za kiuchumi zinazosababishwa na virusi vya corona. (Mail)

Real pia wanafikiria kuwauza wachezaji mpaka sita wa kikosi cha kwanza, akiwemo winga wa Wales Gareth Bale, 30 na kiungo James Rodriguez, 28. (AS)NeymarPSG inajipanga kumbakiza Neymar klabuni hapo mpaka 2025

Paris St-Germain wanaandaa mkataba mpya mpaka mwaka 2025 kwa ajili ya mshambuliaji wa Brazili Neymar. Neymar, 28 atapata kitita cha euro milioni 38 (pauni milioni 33) kwa mwaka. (Sport – in Spanish)

Arsenal na Manchester United wanafikiria kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele,22. (Sport – in Spanish)Kai HavertzMan United wanataka kumsajili kiungo kinda wa Ujerumani Kai Harvertz

Manchester United wamemuongeza kiungo wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz,20, kwenye orodha yao ya wachezaji watakaotaka kuwasajili. (Standard)

Arsenal wanaweza kumtoa mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette, 28 kwenda Atletico Madrid kama sehemu ya makubaliano ili kumpata kiungo wa kati wa Ghana Thomas Party ,26. (Sun)Rodrigo MorenoArsenal wamuulizia rasmi Moreno

Arsenal wameulizia rasmi uwezekano wa kumsajili winga wa Valencia na Uhispania Rodrigo Moreno, 29. (Mirror)

The post Juventus wahamia kwa Harry Kane, Madrid kuwauza wachezaji wake nyota 6 kisa mtikisiko wa kiuchumi appeared first on Bongo5.com.