Maafisa wa afya wa jiji la Wuhan lililokuwa kitovu cha mlipuko wa janga la virusi vya corona wametangaza kutokuwa na mgonjwa yoyote aliyelazwa hospitalini kutokana na maradhi yanayosambazwa na virusi hivyo na hiyo itakuwa ni kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa kwa mlipuko wa COVID-19.

A man wearing a face mask arrives to buy vegetables at a stall in Wuhan in China's central Hubei province on April 18.

Mtu aliyrvalia maski akionekana sokoni akinunua mboga katika jiji la Wuhan nchini China picha ya Aprili 18.

Kulingana na msemaji wa tume ya kitaifa ya afya nchini China, Mi Feng aliyezungumza na waandishi wa habari hii leo, taarifa hii ya karibuni zaidi inaonyesha hakuna maambukizi yoyote ya virusi vya corona kwenye jiji hilo, na kupongeza hatua za pamoja kati ya Wuhan na wahudumu wa afya kutoka maeneo mbalimbali nchini humo.

Jiji hilo liliripoti juu ya watu 46,452 wanaougua homa ya mapafu COVID-19 sawa na asilimia 56 ya maambukizi yote nchini China. Watu 3,869 walifariki dunia.

The post Jiji la Wuhan latangaza kutokuwa na mgonjwa yoyote wa Virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.